Moja kwa moja , Trump atishia Iran huku jeshi la IRGC likilenga rada za Marekani Bahrain
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran limesema limelenga na kuharibu rada ya tahadhari ya mapema nchini Bahrain, likijibu shambulio la anga lililofanyika usiku wa manane katika eneo la Sirik.
Muhtasari
Trump atishia kuishambulia Iran
Moja kwa moja
Na Beldeen Waliaula
Hakuna kitakachosalia Iran iwapo watawalenga viongozi wa Marekani -Trump
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya Donald Trump
Katika
mahojiano na shirika la habari la Salem News, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kutumia tena
nguvu za kijeshi dhidi ya Iran na iwapo angesita kuchukua hatua hiyo, Rais wa
Marekani Donald Trump alijibu
kuwa akiona mwelekeo wa mambo unabadilika, atachukua hatua bila kusita.
"Ikiwa
nitaona mambo yanaelekea upande tofauti, nitafanya hivyo. Huenda nikafanya
hivyo hata sasa hivi. Bila kusita hata kidogo," alisema Trump .
Alipoulizwa
iwapo kuendelea kuwepo
kwa serikali ya Iran madarakani hadi atakapomaliza muhula wake katika Ikulu ya
White House kutamaanisha ameshindwa katika vita
hivyo, Trump alijibu,
"Ndiyo, huo utakuwa ni ushindi wa Iran na kushindwa upande wangu.”
Akijibu
swali kuhusu hatua ambayo Washington ingechukua iwapo Iran ingemuua kiongozi wa
ngazi ya juu wa Marekani, Trump alisema, "Basi hakutakuwa na chochote
kitakachosalia kwao."
Aidha, Iran imetishia kuwa iwapo
itashambuliwa tena kijeshi, haitafungia mipaka ya mzozo huo katika eneo la
Mashariki ya Kati pekee, bali itashambulia
kambo zote za kijeshi za Marekani zilizo bara Asia na Ulaya.
Naweza kuharibu miundombinu yote ya Iran ndani ya siku tatu - Trump
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha ya Donald Trump
Rais
wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Saudi Arabia, Qatar, Falme za Kiarabu na mataifa mengine ya Ghuba
yamemuomba asitishe kwa sasa kutekeleza mashambulizi makubwa dhidi ya Iran.
Trump
amedai kuwa kama si ombi hilo, angeweza kuharibu miundombinu ya nishati ya
Iran, madaraja na viwanda vyake ndani ya siku tatu.
Katika mahojiano aliyoyafanya hapo jana, Trump
alisema ana uwezo wa kumaliza vita hivyo, lakini kutokana na ombi la
washirika wa Marekani katika eneo hilo, ameendelea kuiwekea Iran shinikizo la
kiuchumi na kijeshi.
"Saudi
Arabia imeniomba niache hali iendelee kama ilivyo kwa muda fulani,"
alisema Trump.
Alipoulizwa
iwapo angefanya mashambulizi zaidi dhidi ya Iran kama asingepokea maombi hayo,
Trump alijibu, "Ndiyo, ningefanya
hivyo."
Rais
huyo wa Marekani alikiri kuwa hadi sasa Washington imejizuia kwa kiasi kikubwa
kulenga miundombinu ya nishati na madaraja nchini Iran.
"Ndani
ya siku moja, vyanzo vyao vya nishati vitakuwa vimeharibiwa. Ndani ya siku
moja, madaraja yao yatakuwa yameharibiwa, na ndani ya siku moja, uwezo wao wa
uzalishaji viwandani utakuwa umeharibiwa. Mambo hayo yatachukua siku tatu
pekee," alisema.
Trump
pia alikiri kuwa kupanda kwa bei ya petroli kufuatia vita hivyo kulichangia
kushindwa kwa chama cha Republican katika uchaguzi wa katikati ya muhula.
Hata
hivyo, alitetea uamuzi wake wa kuishambulia Iran.
Tetesi za soka Ulaya: Man United na Man City zapigana vikumbo kwa Malo Gusto
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United na Manchester City wanajiandaa kuwania saini ya beki wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Malo Gusto, mwenye umri wa miaka 23. (Talksport)
Liverpool wamemuweka katika orodha ya wachezaji wanaowafuatilia beki wa Brighton, Luka Vuskovic, mwenye umri wa miaka 19, kwa ajili ya usajili wa majira yajayo ya kiangazi. Hata hivyo, Brighton wanadaiwa kumuwekea thamani ya takribani pauni milioni 80. (Florian Plettenberg)
Fulham wanaongoza katika mbio za kuwania saini ya winga wa Real Betis ya Hispania, Rodrigo Riquelme, mwenye umri wa miaka 26. (Teamtalk)
Everton wanaweza kujaribu kumsajili kiungo wa Tottenham Hotspur, Conor Gallagher, mwenye umri wa miaka 26, iwapo klabu hiyo ya kaskazini mwa London itaamua kumuuza katika dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)
PSV Eindhoven ya Uholanzi imeanza mazungumzo na Napoli kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne, mwenye umri wa miaka 35, katika dirisha la Januari. (Il Mattino – kwa Kiitaliano)
Kiungo wa AC Milan, Youssouf Fofana, mwenye umri wa miaka 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Sevilla, anafuatiliwa na Tottenham Hotspur na Juventus. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)
Kocha wa Charlotte FC ya Marekani, Dean Smith, anataka kuungana tena na kiungo mshambuliaji Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 31, ambaye aliwahi kufanya naye kazi Aston Villa. Hata hivyo, mshahara wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England, ambaye kwa sasa yuko Everton kwa mkopo akitokea Manchester City, unaweza kuwa kikwazo katika mpango huo. (Football Insider)
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Folarin Balogun
Mshambuliaji wa Monaco na timu ya taifa ya Marekani, Folarin Balogun, mwenye umri wa miaka 25, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolengwa na Mauricio Pochettino kwa ajili ya usajili wake wa kwanza akiwa kocha wa Manchester United. Balogun aliwahi kukaribia kujiunga na Everton siku ya mwisho ya dirisha la usajili majira yaliyopita. (Teamtalk)
Leeds United ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Middlesbrough na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Will Lankshear, mwenye umri wa miaka 21. Mchezaji huyo amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipojiunga na Middlesbrough akitokea Tottenham Hotspur katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football Insider)
Newcastle United na Sunderland zinafuatilia maendeleo ya kiungo wa Sheffield United na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Sydie Peck, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anatajwa kuwa na kipaji kikubwa. (Teamtalk)
Tottenham Hotspur inafikiria kuvunja mkataba wa mkopo wa winga wake Mikey Moore, mwenye umri wa miaka 19, anayeichezea Cologne ya Ujerumani. Hatua hiyo inaweza kumfungulia njia ya kurejea Rangers ya Scotland katika dirisha la Januari. (Teamtalk)
Barcelona haina mpango wa kumuuza kiungo wake Gavi, mwenye umri wa miaka 22, licha ya kuwepo kwa taarifa za Bayern Munich na Napoli kutaka kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania. (Marca – kwa Kihispania)
Iran yashambulia kituo cha kijeshi cha Marekani Bahrain
Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi
la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), katika taarifa iliyotolewa leo
asubuhi,imesema kuwa, "imelenga
na kuharibu" rada ya kutoa
tahadhari za mapema ya majeshi ya Marekani
nchini Bahrain, ikiwa
kama jibu la shambulio la anga la ambalo Marekani ilitekeleza
eneo la Sirik.
Katika
taarifa hiyo, IRGC imesema, "Hili ni onyo kali kwa adui kusitisha vitendo vyake vya uchochezi angani
na na kujaribu kupitisha mafuta kimagendo
katika Mlango-Bahari wa Hormuz.”
“Endapo ukiukaji wa mipaka na
uchokozi huo utajirudia, kikosi cha anga cha IRGC kiko tayari kwa makabiliano yasiyo na mipaka.”
Saa
moja kabla ya kutolewa kwa tangazo hilo, mashirika ya habari ya Iran yalikuwa
yameripoti shambulio la anga katika eneo la Sirik.
Baadaye,
jeshi la IRGC ,lilithibitisha
shambulio hilo na kusema kuwa mnara wa mawasiliano katika eneo hilo, lililoko
karibu na pwani ya Ghuba ya Uajemi, ulikuwa miongoni mwa maeneo yaliyolengwa
katika mashambulizi hayo.
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja Ijumaa ya leo