Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja , Marekani imepata pigo la kihistoria baada ya ushindi wa Democrats - Trump

Rais Trump amesema kuwa huenda sera zake za kuwafukuza wahamiaji “zilikuwa kali kupita kiasi” haswa kwa watu ambao wameishi zaidi ya mwongo mmoja nchini Marekani.

Muhtasari

Marekani imepata pigo la kihistoria baada ya ushindi wa Democrats - Trump

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Watu 7 wafariki, zaidi ya 100 wajeruhiwa katika ajali ya treni nchini Misri

    Takriban watu saba wamefariki dunia katika ajali ya treni iliyotokea karibu na mji wa Giza nchini Misri, huku watu wengine zaidi ya100 wakijeruhiwa.

    Mamlaka ya reli nchini humo imesema treni mbili zilizokuwa zikielekea maeneo ya kusini kutoka Giza na Cairo ziligongana, na kusababisha mabehewa kadhaa kuacha njia na kuanguka.

    Picha za eneo la ajali zinaonyesha watu wakichunguza ndani ya mabehewa yaliyopinduka kuwatafuta abiria waliojeruhiwa, huku operesheni kubwa ya uokoaji ikiendelea.

    Rais wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi, amesema anazitaka mamlaka za serikali kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuwaajibisha wote watakaopatikana na utepetevu kazini.

    Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma imeonya kuwa idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka.

  2. Tetesi za usajili Ulaya: Man Utd yamtaka Murillo, Carrick akalia kuti kavu

    Manchester United inaweza kuandaa ofa kubwa kwa ajili ya kumsajili beki wa kati wa Nottingham Forest, Murillo, 24, katika dirisha la usajili la majira ya joto. (Football Insider)

    Manchester United ikiamua kumfuta kazi kocha wake Michael Carrick, 45, aliyekuwa kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, 48, na aliyewahi kuzinoa timu za taifa za Ujerumani, Bayern Munich na RB Leipzig, Julian Nagelsmann, 39, wanatajwa kuwa miongoni mwa wagombea wakuu wa nafasi hiyo. (Manchester Evening News)

    Hata hivyo, kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino, ambaye aliwahi kuzinoa Tottenham na Chelsea, ndiye anayetajwa na kampuni za ubashiri kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kurithi mikoba ya Carrick iwapo ataondoka Old Trafford. (The Standard)

    Liverpool, Manchester United na Chelsea ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England zinazofuatilia kiwango cha beki wa kati wa AC Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji, Koni de Winter, 24. (Caught Offside)

    Everton, Chelsea, Manchester United na Tottenham zimewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Vitor Roque, 21, ambaye ni raia wa Brazil. Palmeiras inatajwa kumthaminisha kwa pauni milioni 42. (Bolavip kupitia Teamtalk)

    Manchester United ilifanya mawasiliano na Manchester City kuhusu uwezekano wa kumsajili beki Rayan Ait-Nouri, 25, katika dirisha la majira ya joto. Klabu hiyo inaweza kurejea tena kumuwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria katika dirisha la Januari. (Football Insider)

    Brentford, Chelsea, Fulham, Manchester City, Newcastle United na Tottenham ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia beki wa Lens na Ufaransa, Ismaelo Ganiou, 21. (Teamtalk)

    Liverpool nayo inatarajiwa kusubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua iwapo itamsajili moja kwa moja beki wa Barcelona, Ronald Araujo, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Anfield.

    Chelsea, Inter Milan na Al-Hilal zimeweka kwenye rada kiungo wa Aston Villa na timu ya taifa ya Ufaransa, Boubacar Kamara, 26, baada ya kurejea uwanjani kufuatia jeraha lililomuweka nje ya mchezo. (Fussball News)

    Liverpool na beki wa Uruguay, Ronald Araujo, 27, wanatarajia kusubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua kuhusu uwezekano wa kuendeleza mkataba wake kwa dau la pauni milioni 47. Araujo yuko Liverpool kwa mkopo akitokea Barcelona. (Sport)

    Everton inaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa Ivory Coast, Abdoulaye Doumbia, 19, kutoka klabu ya BK Hacken ya Sweden. Sunderland na Coventry City pia zinatajwa kumuwania mchezaji huyo. (Football Insider)

    Everton inavutiwa na mshambuliaji Kelvin Yeboah, 26, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mshambuliaji wa Leeds United, Tony Yeboah. Klabu hiyo inatajwa kutaka kumsajili katika dirisha la Januari baada ya kufunga mabao 18 katika mechi 32 akiwa na Minnesota United ya Marekani msimu huu. (The Hard Tackle)

    Crystal Palace na Ipswich Town zimejiunga na Everton katika mbio za kumuwania Kelvin Yeboah, ambaye klabu yake ya sasa, Palmeiras, inatajwa kumthaminisha kwa pauni milioni 42. (Football Insider)

  3. Marekani imepata pigo la kihistoria baada ya ushindi wa Democrats - Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema hapo jana kuwa Marekani "imerudi nyuma kihistoria", huku Ikulu ya White House ikiendelea kukumbwa na misukosuko kufuatia mabadiliko ya uongozi yaliyofanyika baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula.

    Miongoni mwa mabadiliko hayo ni tangazo lake kwamba Stephen Miller atachukua nafasi ya mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu kutoka kwa Susie Wiles.

    Trump alifanya mahojiano yake ya kwanza ya moja kwa moja baada ya uchaguzi huo na kipindi cha 60 Minutes ambapo alisema huenda sera zake za kuwafukuza wahamiaji “zilikuwa kali kupita kiasi” haswa kwa watu ambao wameishi Zaidi ya mwongo mmoja nchini Marekani.

    Trump aliongezea kuwa kuwa msako dhidi ya wahamiaji "ulimsaidia na pia kumdhuru" katika uchaguzi huo. Ila alisisitiza kuwa wengi wanamsifia kwa kuwaondoa wahalifu nchini humo na kufunga mipaka ya taifa hilo

  4. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja Jumatatu ya leo