Moja kwa moja , Iran yatishia kumuua Trump na Netanyahu

Naibu Mkuu wa Majeshi ya Iran, ametishia kuwaua viongozi wa Marekani na Israel katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini humo.

Muhtasari

Iran yastishia kumuua Trump na Netanyahu

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Arsenal, Chelsea, Liverpool vyamgombania Alex Scott wa Bournemouth

    Arsenal wameungan na Chelsea na Liverpool katika mbio za kumtaka kiungo wa kati wa Bournemouth, Alex Scott, mwenye umri wa miaka 23, raia wa England. Vilabu hivyo vimewasiliana na Bournemouth kuulizia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo ambaye mkataba wake unamalizika majira ya kiangazi mwaka 2028. (i Sport)

    Iwapo Mauricio Pochettino atateuliwa kuwa meneja wa Manchester United, Shirikisho la Soka la Marekani linataka aliyekuwa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, achukue nafasi yake kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanaume ya Marekani. (Talksport)

    Chelsea, Real Madrid na Atletico Madrid zinafuatilia kwa karibu hali ya kiungo wa Arsenal, Martin Zubimendi, mwenye umri wa miaka 27, zikiwa na matumaini ya kumsajili raia huyo wa Hispania katika dirisha la usajili la Januari. (Independent)

    Hata hivyo, Zubimendi amesema ana furaha kuishi London na ameshangazwa na tetesi zinazomhusisha na kuondoka Arsenal. Anasema hajawasiliana na mtu yeyote kuhusu uwezekano wa kuhamia klabu nyingine. (Marca - in Spanish)

    Liverpool inaandaa mkataba mpya kwa kiungo wake chipukizi Trey Nyoni, mwenye umri wa miaka 19, kama zawadi kwa kiwango kizuri alichoonyesha msimu huu. Nyoni, ambaye ni kiungo wa timu ya taifa ya England ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20, amekuwa akifanya vizuri na klabu hiyo inataka kumhakikishia mustakabali wake. (GiveMeSport)

    Manchester United imeongeza majina ya mabeki wawili katika orodha ya wachezaji inayowafuatilia kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi. Wachezaji hao ni Nathan Collins, mwenye umri wa miaka 25, anayeichezea Brentford na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, pamoja na Calvin Bassey, mwenye umri wa miaka 26, raia wa Nigeria anayeichezea Fulham.

    Wawili hao wameongezwa katika orodha ambayo tayari inamjumuisha beki wa Everton na timu ya taifa ya England, Jarrad Branthwaite, mwenye umri wa miaka 24. (Mail

    Calvin Bassey

    Bournemouth, Everton na Nottingham Forest zote zinawania saini ya mshambuliaji wa Vasco da Gama, Andres Gomez, mwenye umri wa miaka 24. Klabu hiyo ya Brazil inathamini mkataba wa mshambuliaji huyo kwa takribani pauni milioni 17. (ESPN)

    Brentford iko tayari kukataa ofa zote zitakazowasilishwa na Liverpool kwa ajili ya kumsajili beki wake wa kushoto El Hadji Malick Diouf, mwenye umri wa miaka 21. (Football Insider)

    Aston Villa inafikiria kumsajili kiungo wa Chelsea, Romeo Lavia, mwenye umri wa miaka 22. Kocha wa Villa, Unai Emery, anatajwa kuwa na kuvutiwa sana na kiungo huyo raia wa Ubelgiji. (Fussball News via Teamtalk), external

    Juventus inalenga kumsajili kwa mkopo beki wa kushoto wa Manchester City na timu ya taifa ya Algeria, Rayan Ait-Nouri, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha la usajili la Januari. (Gazzetta dello Sport)

    Hata hivyo, Barcelona nayo inamtaka Ait-Nouri, huku beki wake wa kushoto Alejandro Balde, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Hispania, akitajwa kuwa huenda akaondoka klabuni hapo katika dirisha la usajili la majira ya baridi. (Sport - in Spanish), external

    Beki wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Levi Colwill, mwenye umri wa miaka 23, anavutiwa na Barcelona, lakini Chelsea imesisitiza kuwa haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo. (Football Insider)

  2. Wahispania waandamana kupinga gharama ya maisha na makazi

    .

    Mapigano yamezuka kati ya makundi ya watu waliovalia barakoa na polisi mjini Barcelona baada ya makumi ya maelfu ya watu kushiriki mgomo mkuu wa kwanza nchini Uhispania baada ya miaka 14.

    Mgomo huo uliitishwa na vyama vikuu vya wafanyakazi nchini humo kupinga hali duni ya makazi na gharama ya juu ya maisha.

    Takriban watu 120,000 walishiriki katika maandamano hayo, katika mji mkuu wa Madrid, huku zaidi ya watu 50,000 wakijitokeza mjini Barcelona.

    Picha za video zilionyesha wanaume waliovalia barakoa wakichoma moto mapipa ya taka na kuvunja vioo vya maduka huku polisi wakitumia vitoa machozi kuwatawanya.

    Huduma za usafiri na huduma nyingine za umma kote nchini Uhispania ziliathirika kutokana na mgomo huo.

    Wahispania wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa ubunge utakaofanyika tarehe 29 mwezi Novemba.

    Soma pia:

  3. Iran yatishia kumuua Trump na Netanyahu

    .

    Brigedia Jenerali Kiomars Heidari, Naibu Mkuu wa Majeshi ya Iran, ametishia kuwaua viongozi wa Marekani na Israel katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini humo.

    "Tutamuua Trump na Netanyahu," alisema afisa huyo wa kijeshi katika video iliyochapishwa na shirika la habari la serikali ya Iran hapo jana

    Katika mahojiano hayo, mwanajeshi huyo, alidai kuwa meli zote za kivita za Marekani kwa sasa zimewekwa katika umbali wa kilomita 500 kutoka Iran.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya vikosi vya Iran kulenga meli mbili za kivita za Marekani tarehe 6 na 7 mwezi Septemba.

    Naibu Mkuu huyo wa Majeshi ya Iran pia alidai kuwa wakati wa mzozo wa kijeshi katika miezi iliyopita, vikosi vya Iran viliweza kuangamiza ndege 300 za Marekani, pamoja na kuteka baadhi ya ndege hizo kwa kutumia mifumo ya vita vya kielektroniki.

    Aidha, alionya kuwa kuna siri kubwa ya makombora ambayo imefichwa, na iwapo vita vitazuka tena watafichua siri hiyo.

    Soma pia:

  4. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja Alhamisi ya leo