Arsenal, Chelsea, Liverpool vyamgombania Alex Scott wa Bournemouth
Arsenal wameungan na Chelsea na Liverpool katika mbio za kumtaka kiungo wa kati wa Bournemouth, Alex Scott, mwenye umri wa miaka 23, raia wa England. Vilabu hivyo vimewasiliana na Bournemouth kuulizia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo ambaye mkataba wake unamalizika majira ya kiangazi mwaka 2028. (i Sport)
Iwapo Mauricio Pochettino atateuliwa kuwa meneja wa Manchester United, Shirikisho la Soka la Marekani linataka aliyekuwa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, achukue nafasi yake kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanaume ya Marekani. (Talksport)
Chelsea, Real Madrid na Atletico Madrid zinafuatilia kwa karibu hali ya kiungo wa Arsenal, Martin Zubimendi, mwenye umri wa miaka 27, zikiwa na matumaini ya kumsajili raia huyo wa Hispania katika dirisha la usajili la Januari. (Independent)
Hata hivyo, Zubimendi amesema ana furaha kuishi London na ameshangazwa na tetesi zinazomhusisha na kuondoka Arsenal. Anasema hajawasiliana na mtu yeyote kuhusu uwezekano wa kuhamia klabu nyingine. (Marca - in Spanish)
Liverpool inaandaa mkataba mpya kwa kiungo wake chipukizi Trey Nyoni, mwenye umri wa miaka 19, kama zawadi kwa kiwango kizuri alichoonyesha msimu huu. Nyoni, ambaye ni kiungo wa timu ya taifa ya England ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20, amekuwa akifanya vizuri na klabu hiyo inataka kumhakikishia mustakabali wake. (GiveMeSport)
Manchester United imeongeza majina ya mabeki wawili katika orodha ya wachezaji inayowafuatilia kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi. Wachezaji hao ni Nathan Collins, mwenye umri wa miaka 25, anayeichezea Brentford na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, pamoja na Calvin Bassey, mwenye umri wa miaka 26, raia wa Nigeria anayeichezea Fulham.
Wawili hao wameongezwa katika orodha ambayo tayari inamjumuisha beki wa Everton na timu ya taifa ya England, Jarrad Branthwaite, mwenye umri wa miaka 24. (Mail
Bournemouth, Everton na Nottingham Forest zote zinawania saini ya mshambuliaji wa Vasco da Gama, Andres Gomez, mwenye umri wa miaka 24. Klabu hiyo ya Brazil inathamini mkataba wa mshambuliaji huyo kwa takribani pauni milioni 17. (ESPN)
Brentford iko tayari kukataa ofa zote zitakazowasilishwa na Liverpool kwa ajili ya kumsajili beki wake wa kushoto El Hadji Malick Diouf, mwenye umri wa miaka 21. (Football Insider)
Aston Villa inafikiria kumsajili kiungo wa Chelsea, Romeo Lavia, mwenye umri wa miaka 22. Kocha wa Villa, Unai Emery, anatajwa kuwa na kuvutiwa sana na kiungo huyo raia wa Ubelgiji. (Fussball News via Teamtalk), external
Juventus inalenga kumsajili kwa mkopo beki wa kushoto wa Manchester City na timu ya taifa ya Algeria, Rayan Ait-Nouri, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha la usajili la Januari. (Gazzetta dello Sport)
Hata hivyo, Barcelona nayo inamtaka Ait-Nouri, huku beki wake wa kushoto Alejandro Balde, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Hispania, akitajwa kuwa huenda akaondoka klabuni hapo katika dirisha la usajili la majira ya baridi. (Sport - in Spanish), external
Beki wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Levi Colwill, mwenye umri wa miaka 23, anavutiwa na Barcelona, lakini Chelsea imesisitiza kuwa haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo. (Football Insider)