Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu, amekuwa akikabiliwa na kesi hiyo tangu Oktoba mwaka 2025, akituhumiwa kuchochea uasi na kudhoofisha mamlaka ya serikali.
HECHE: Hukumu ya Lissu ni ishara ya ushindi kwa Chadema
Maelezo ya picha, John Heche
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amesema kuondolewa kwa shtaka la uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, na badala yake kutiwa hatiani kwa kosa la uchochezi ni ishara ya ushindi kwa chama hicho na Watanzania.
Heche ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, baada ya Mahakama Kuu kumhukumu Lissu kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la uchochezi, kufuatia kushindwa kwa upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka la uhaini lililokuwa likimkabili.
Amesema Lissu na viongozi wengine ni sehemu tu ya harakati za chama hicho, akisisitiza kuwa CHADEMA kina viongozi wa kutosha kuendeleza mikakati yake bila kuyumbishwa na changamoto zinazowakabili baadhi ya viongozi wake.
Kwa upande wake, CHADEMA imetangaza nia ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo, huku ikiendelea kutafuta uwezekano wa Lissu kupata dhamana wakati akisubiri hatua za rufaa.
'Tulitamani awe huru amzike kaka yake"- Dada wa Lissu
Chanzo cha picha, screengrab
Dada wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Rose Masesa, amesema familia ilitamani kumuona Lissu akiwa huru ili aweze kushiriki mazishi ya kaka yao Alute Lissu Mughwai, lakini licha ya kutotimia kwa matarajio hayo, hawajakata tamaa.
Akizungumza baada ya hukumu ya kifungo cha miaka minne iliyotolewa dhidi ya Lissu, Rose amesema familia ilifika mahakamani kumuonesha mshikamano katika kipindi chote cha kesi hiyo.
“Tuliamua kuja kuonesha solidarity, tuko na Tundu mpaka dakika ya mwisho. Pamoja na machungu ya familia tuliyopitia, tumemtia nguvu. Najua ametuona na tuko pamoja naye,” amesema.
Rose amesema familia ilitarajia Lissu angeachiwa huru ili apate fursa ya kushiriki mazishi ya kaka yao aliyefariki wiki hii, akieleza kuwa kutokuwepo kwake katika tukio hilo ni miongoni mwa machungu waliyopitia.
Akizungumzia hukumu hiyo, amesema yaliyotokea yamewafanya kutafakari hali ya haki na mwenendo wa taifa, akidai kuwa wamejifunza kuwa mtu anaweza kunyimwa haki bila sababu.
“Tumejua nchi yetu iko katika hali gani, tumejua tunapita katika kipindi gani na taifa letu sasa hivi likoje. Tumejua kwamba kumbe inawezekana mtu akanyimwa haki tu bila sababu,” amesema.
Hali ilivyokuwa ndani na nje ya Mahakama hukumu ya Lissu
Picha mbalimbali kuonyesha hali ilivyokuwa nje na ndani ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam wakati wa hukumu ya kesi ya uhaini iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu
Lissu akosoa hukumu asema ni ya kisiasa
Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya hukumu kwamba Lissu hana hatia ya kosa la uhaini lakini amekutwa na kosa la uchochezi, Lissu anazungumza
Lissu: Naomba mnisikilze kwa makini kama ambavyo mmekua mkinisikiliza, leo ni siku ya 577, kwa kuitwa mhaini, kosa ambalo kwa Katiba ya nchi yetu ndiyo kosa kubwa kuliko yote katika Jamuhuri ya Muungano, ndiyo kosa pekee lililotamkwa katika katiba-uhaini.
Kwa siku 577, nimeitwa mhanini kwa mujibu wa kifungu niliposhitakiwa nacho cha 39 2 (d) adhabu yake inaweza kuwa kifo.
Baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la kifo kuning'inia juu ya kichwa changu, leo waheshimiwa majaji mmeniita mchochezi kosa ambalo wala halina adhabu, halijapangiwa adhabu.
Mmeniita mchochezi na wakili wa serikali mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini, maana yake ni nini waheshimiwa majaji, kosa nililoshitakiwa nalo halikuwa kisa na leo mmesema hilo halikuwa kosa kwa hiyo nilikaaa siku 577 bila kosa lolote.
Waheshimiwa majaji kauli yenu kuwa halikuwa kosa imekubaliana na kauli yangu na msimami wangu kwamba halikuwa kosa.
Kuna kitu kimoja hamjakisema na ntakisema kwa rekodi na ushahidi wangu umethibitisha hilo. Hii ilikuwa kesi ya kisiasa kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa kwa hukumu yenu ya kisiasa mmethibitisha hilo, kwa sababu inabidi visababu vitengenezwe vya kumfunga mgomvi wetu wa kisiasa, sababu zitafuwe za kumfuga huyu mpinzani wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo majaji mmetengeneza sikushitakiwa kwa uchochezi.
Na kwa heshima kubwa mmefanya hivyo kwa sababu za kisiasa kwa sababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe tu hivi akaona ameshinda serikali itaabika kwa hiyo tafuteni vijisababu, ndicho mlichofanya leo waheshimiwa majaji na ninajua mnahukumu na ninajua niaisikia moyoni, I feel it in my heart kwa bahati mbaya majaji mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Mzee Jomo Kenyata mwaka 1954.
Mahakama yaona ushahidi haujathibitisha nia ya Lissu kutenda uhaini
Mahakama Kuu imeeleza kuwa upande wa mashtaka haujatoa ushahidi unaothibitisha kuwa Tundu Lissu alikuwa na nia ya kutenda kosa la uhaini kwa kuchochea umma kuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia serikali.
Nia ya kutenda kosa ni moja ya viini vitatu ambavyo Mahakama imejielekeza kuamua kesi hiyo ya uhaini inayomkabili Lissu.
Katika kuchambua kiini cha tatu cha kosa hilo, mahakama imeeleza kuwa haijaona ushahidi wa kuthibitisha nia hiyo.
Katika kuchambua kiini cha kwanza kuhusu utii, mahakama imeona kuwa Lissu alikuwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), baada ya yeye mwenyewe kukiri kuwa ni raia na mzaliwa wa Tanzania.
Kuhusu kiini cha pili, kinachohusu iwapo Lissu alikuwa na nia ya kuhamasisha umma kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia serikali, mahakama imesema haijaona ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha nia hiyo. Imeeleza kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka haujakidhi kiwango kinachohitajika kuthibitisha kiini hicho cha kosa la uhaini.
Hata hivyo, mahakama imeelekeza kwenye kifungu cha 319(1) na (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinachoeleza uwezo wa mahakama kubadilisha shitaka na kutoa uamuzi kuhusu kosa dogo zaidi pale ushahidi unapothibitisha uwepo wa kosa hilo.
Mahakama Kuu nchini Tanzania, imetupilia mbali pingamizi la Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, lililokuwa likipinga uhalali wa hati ya mashtaka katika kesi yake ya uhaini, ikisema hati hiyo inakidhi matakwa yote ya kisheria.
Katika hoja zake za mwisho, Bw. Lissu aliiomba mahakama imuachie huru, akidai kuwa hati ya mashtaka haikuwa na maelezo ya kutosha kumwezesha kuandaa utetezi wa kina dhidi ya tuhuma zinazomkabili.
Miongoni mwa hoja alizozitoa, alipinga matumizi ya neno "umma" katika hati ya mashtaka, akisema sheria inayotumika katika shtaka hilo inazungumzia kushawishi mtu au kundi la watu, na si umma kwa ujumla.
Hata hivyo, Jaji Dunstan Ndunguru, anayeliongoza jopo la majaji watatu wanaosikiliza shauri hilo, alikubaliana na hoja za upande wa mashtaka kwamba neno "umma" linajumuisha watu binafsi pamoja na makundi ya watu, hivyo matumizi yake katika hati ya mashtaka hayakuwa na kasoro yoyote ya kisheria.
Mahakama ilisema hati ya mashtaka ina maelezo ya kutosha kumfahamisha mshtakiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili na kumwezesha kuandaa utetezi wake ipasavyo.
"Kwa sababu hiyo, pingamizi hili halina mashiko na mahakama inalitupilia mbali," alisema Jaji Ndunguru wakati akisoma uamuzi huo.
Baada ya kutupilia mbali pingamizi hilo, mahakama iliendelea kuchambua vipengele vya kisheria vinavyounda kosa la uhaini, ili kubaini iwapo upande wa mashtaka umefanikiwa kuthibitisha masharti muhimu ya kosa analodaiwa kutenda Bw. Lissu.
Tayari Jaji Dunstan Ndunguru ameanza kutoa maelezo kuelekea hukumu..
Ndunguru: Maelezo yanasema kwamba
tarehe tatu ya mwezi wa nne 2025 katika Wilaya ya Kindondoni mshitakiwa akiwa kwenye utii wa Jamuhuri wa Muungano alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi wa mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali kwa kutamka … 'Ni kweli sababu tutaahamasisha uasi … tunaenda kukinukisha sana sana tutauvuruga huu uchaguzi'
Mshitakiwa aliposomewa mashitaka alikana na shauri likawa tayari kusikilizwa. Wenye wajibu wa kuthibitisha ni mawakili wa serikali ambao ni ni Nasoro Katuga na wenzake. Na upande wamashitaka walileta mashahidi 17 wakiwemo mashihidi wa kificho kwa mujibu wa sheria. Mshitakiwa alijiwakilisha mwenyewe na kuleta mashahidi pamoja na kuleta vielelezo ambayo ni maelezo ya mashitaka namba moja hadi 16 na mshitakiwa alijitetea na mwisho pande zote zilileta hoja za mwisho kwa pande zote mbili kwa maana ya hoja za majumuisho yani fainal submission.
Jaji Ndunguru anaendelea kusoma hukumu:
Nduguru: Sasa Mahakama hii imepitia hati ya mashitaka, ushahidi pande zote mbili na pia imezingatia majumuisho ya mwisho na mahakama imejikita ina viini vitatu vinavyotakiwa kuthibitishwa.
1. Je mshitakiwa alikuwa chini ya utii wa Jamuhuri ya Muungano
2. Ni iwapo mshitakiwa alitemgeneza nia ya kuitishia serikali kwa kuzuia uchaguzi mkuu
3. Ni iwapo mshitakiwa alidhihirisha jia hiyo kwa kuchapisha
Ni vyema kabla hatujaendelea tutoe ufafanuzi juu ya hoja za mwisho kwenye hati ya mashitaka, kabla hatujaenda kwenye hatua ya kusoma hukumu.
Mshitakiwa alisema hati ya mashitaka ina mapungufu kwenye maeneo matatu. Mshitakiwa alisema kwa mujibu wa husika inazungumzia kikundi cha watu na hati inasema kuchochea uma.
Kuna tofauti kwenye lengo na vile kifungu cha pili D. Mahakama hii inaomba iwakumbushe kuwa swala hati ya mashitaka lilishaletwa pia kwenye Mahakama hii hatua zza mwanzoni na ikaamua Septemba 20/25 kwamba hati hiyo ilikuwa sahihi, hata hivyo kwa kuwa hoja hiyo imekuja tena Mahakama imeona ni vyema Mahakama ikatoa ufafanuzi.
Mshitakiwa aliieleza Mahakama kwamba, kifungu husika kunazungumzia kuhamasisha kikundi cha watu na hati ya mashitska imeeleza neno 'public' (umma) hivyo upande wa Mashitaka walipaswa kusema ni kina nani hasa? mshitakiwa alisema kwa mapungufu hayo hati hiyo imekinzana na katiba na hivyo haiko kihalali kwa mujibu wa sheria.
Hoja ya pili, mshitakiwa alisema Jamuhuri imeshindwa kuonyesha mtu aliyelengwa kutishiwa na kutolea mfano shauri la Mbowe na wenzake saba. Pia hati ya mashitaka haijaeleza nia hiyo ya kuitishia serikali na anasema maneno yaliyotumika kwenye sheria ndio yangetumika kwenye hati ya mashitaka.
Upande wa mashitaka walisema ni kweli hati ya mashitaka imetumia neno 'public' na hivyo ina maanisha kikundi cha watu na hivyo walitumia neno hilo kimahususi hivyo Mahakama inaona hoja hiyo haina mashiko na hati ya mashitaka iko sahihi na imempa maelezo ya kina kama neno public lilivyotafisiriwa linazungumzia mtu yeyote ndani ya Jamuhuri ya Muungamo wa Tanzania.
Lakini pia tumeangalia kwa makini ushahidi wa upande wa mashitaka na utetezi hivyo tumejiridhisha mshitakiwa alielewa vyema maana ya neno 'public'. Mahakama inaona maelezo yaliyotolewa kwenye hati ya mashikata yamejitosheleza kuelewa neno executive (Serekali) na hatujaona kama kuna utata wowote
Na hoja ya taru upande wa mashitaka lazima waeleze nia mahususi lengo ikiwa ni kutishia serikali na hivyo tunaona mapingamizi yote haya hayana mashiko sababu tulishayatolea maaamuzi.
Sasa kinachofuata ni kuangalia vile viiini nilivyovisoma hapo awali.
Hoja ya kwanza ni endapo mshitakiwa ana utii kwa jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Kuamua hoja hii ni muhimu sababu kuamua shauri la uhaini ni la zima mshitakiwa lazima awe chini ya utii wa Jamuhuri wa Tanzania na jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha kinyume na hapo haliwezi kuthibitika.
Pande zote zinakubaliana kwamba wakati akitenda kosa, alikuwa chini ya utii wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania na katika preliminary hearing pia hili lilithibitishwa na mshitakiwa alikubali yeye ni mtanzania kwa kuzaliwa na ana hati ya kusafiria ya Tanzania na hivyo basi kwa kuzingatia sheria ya mwenyendo wa makosa ya jinai hoja ambazo zinakubalika kwenye mashauri ya awali zinakuwa hazina ukinzani au zina kinga labda Mahakama itamke tofauti.
Hoja ya pili ni kwamba mshitakiwa alikuwa ndani ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania na ni muhimu kuliangalia hilo kuwa tuhuma hizo alizifanya ndani ya Tanzania. Mahakama imeona hoja hiyo ya kwanza haina ubishi na haibishaniwi.
Baada ya kumaliza kiini cha kwanza tuangalie kiini cha pili nacho ni endapo mshitakiwa alitemgeneza nia ya kuhamasisha umma kwa lengo la kuitishia serikali. Upande wa mashitaka wanawajibu wa kuthibitisha nia ovu kwa kutofautisha na kauli za kisiasa na kwa kuwa tunaona nia ni jambo lililo ndani ya mtu hivyo lazima ifafanuliwe na matendo ya mtu na katika shauri hili upande wa mashitaka wanasema mshitakiwa alitamka maneno ambayo yalilenga kuchochea umma kuzuia uchaguzi mwaka 2025 na hivyo kushinikiza serikali kutekeleza mabadiliko ya kisiasa ambayo mashitakiwa alikuwa anayadai.
Kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu amewasili katika Mahakama Kuu.
Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu: Tulifikaje hapa?
Tunapojiandaa kukufahamisha yote yatakayojiri katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Kesi ya Lissu, ufuatao ni msururu wa matukio muhimu kuelekea hukumu hiyo.
Januari 2025: Tundu Lissu achaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA.
Januari - Machi 2025: CHADEMA yaendesha kampeni ya "No Reforms, No Election" kudai mageuzi ya uchaguzi.
3 Aprili 2025: Lissu atoa hotuba ambayo baadaye ikakawa msingi wa shitaka la uhaini.
9 Aprili 2025: Akamatwa mjini Mbinga, mkoani Ruvuma.
10 Aprili 2025: Afikishwa Mahakama ya Kisutu na kushtakiwa kwa uhaini.
2025 - 2026: Kesi yahamia Mahakama Kuu na kusikilizwa kwa miezi kadhaa.
21 Agosti 2026: Mahakama Kuu yaamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu.
Septemba 2026: Lissu akamilisha utetezi wake.
6 Novemba 2026: Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo.
Madai ya kifungo cha miaka 5 kwa Lissu yazua maswali kabla ya hukumu
Chanzo cha picha, Amani Golugwa/Facebook
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kimeeleza wasiwasi kuhusu taarifa zinazodai kuwa kiongozi wake, Tundu Lissu, huenda akahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela katika kesi yake ya uhaini, saa chache kabla ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wake.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Alhamisi mjini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Amani Golugwa, alisema chama hicho kimepokea taarifa kutoka kwa wanaharakati wanaodai kuwa maelezo kuhusu hukumu hiyo yamevuja kabla ya kutolewa rasmi na mahakama.
Golugwa alidai kuwa ikiwa taarifa hizo ni za kweli, kifungo hicho kinaweza kuwa na athari za kisiasa kwa kumzuia Lissu kushiriki uchaguzi wa urais siku zijazo na kutekeleza majukumu yake kama mwenyekiti wa chama.
Alisema madai hayo yamezua wasiwasi miongoni mwa wanachama wa CHADEMA, familia ya Lissu, wanaharakati wa haki za binadamu na baadhi ya waangalizi wa kimataifa wanaofuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Mahakama Kuu haijatoa tamko lolote hadharani kuhusu madai hayo.
Wakati huohuo, polisi wameonekana kuongeza doria na uwepo wao katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kuelekea siku ya hukumu. Jeshi la Polisi limeonya dhidi ya jaribio lolote la kuvuruga amani na kusema linafuatilia taarifa kuhusu watu wanaohamasishwa kusafiri kwenda jijini humo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema watu wote wanaotaka kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo wako huru kufanya hivyo, lakini wanapaswa kuheshimu sheria na taratibu za mahakama.
Lissu amekuwa kizuizini tangu Aprili 2025 baada ya kushtakiwa kwa uhaini kufuatia hotuba aliyoitoa katika mkutano wa CHADEMA jijini Dar es Salaam. Waendesha mashtaka wanadai aliwahamasisha wananchi kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka huo, madai ambayo ameyakanusha.
Katika utetezi wake, Lissu amesema kauli zake zilikuwa sehemu ya mjadala wa kisiasa unaolindwa na katiba na kwamba upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kuthibitisha shtaka la uhaini.
Kesi hiyo imefuatiliwa kwa karibu nchini na kimataifa, huku ikitajwa na baadhi ya makundi ya haki za binadamu kama kipimo muhimu cha hali ya uhuru wa kisiasa na haki nchini Tanzania. Serikali imekuwa ikisisitiza kwamba kesi hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kwamba hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Hukumu ya kesi ya Lissu: Mbivu na mbichi kujulikana leo
Mahakama Kuu nchini Tanzania leo inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa chama cha upinzanicha CHADEMA, Tundu Lissu.
Lissu amekanusha mashtaka yanayomkabili akisema yana msukumo wa kisiasa.
Lissu amekuwa gerezani tangu mwaka wa 2025 baada ya kukamatwa kwenye mkutano wa kisiasa. Waendesha mashtaka wanamtuhumu kwa kuchochea uasi na kuhatarisha usalama wa taifa.
Mwanasiasa huyo alinusurika jaribio la kuuawa mwaka 2017 kabla ya kwenda uhamishoni na baadaye kurejea nchini kuendelea na siasa.
Wafuasi wake, wanaharakati wa haki za binadamu na waangalizi wa kimataifa wanasema hukumu ya leo itakuwa kipimo cha uhuru wa mahakama na hali ya demokrasia nchini.
Serikali, kwa upande wake, inasisitiza kuwa kesi hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria.
Uamuzi wa leo unafuatiliwa kwa karibu ndani na nje ya Tanzania kutokana na athari zake kwa demokrasia na mustakabali wa siasa za nchi hiyo na uhuru wa idara ya mahamaa nchini humo.
Hukumu ya kesi ya Lissu kutolewa tarehe sita Novemba
Kwa ushahidi huu ni wazi kuwa mshtakiwa amesambaza nia yake kwa umma ya kuitishia serikali waheshimiwa majaji tukianza na mashahidi ambao walikuwa washtakiwa kisha baadaye wakaja kuwa mashahidi kifungu cha 151 cha sheria ya ushahidi urekebu wa 2023 kinasema kama hawa mashahidi walikuwa wamechochewa na maneno ya mshtakiwa ni washtakiwa wenza, lakini walikuwa na interest to serve na kwa mujibu wa kifungu hiki hawa ni mashahidi na wako compitent kutoa ushahdii.
Lakini sio tu kuishia kuwa wana interest to serve, je waliona video hawakuona walichocheka hawakuchochewa uzito wake ni kutokana na kile wanachosema na ili kuwadiscredit lazima ku prove wapi walisema uongo.
Waheshimiwa majaji hoja ya mwisho kabisa ilikuwa ni lalamiko kuhusu malalamiko ya ushahidi wa polisi, statement na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Hayo sio contradiction bali ni futher elaboration of the witness. Haya si maneno yangu waheshimiwa.
Mahakama katika kesi ya Abeli Orua alias Matiku dhidi ya Jamuhuri criminial appeal number 421 ilieleza PW4 alitoa ufafanuzi zaidi mahakamani kuelezea zaidi kile alichofikisha kama maelezo polisi na hakukuwa na mpishano wowote.
Waheshimiwa majaji kwa kusema hayo submission yetu ndio hiyo kwa ushahidi wa mashahidi 17 ikiungwa mkono na ushahidi wa mashahidi wa utetezi hivyo tumefanya kazi yetu kwa ukamilifu na ni ombi letu mshtakiwa ahukumiwe sawasawa na shtaka lake.
Nasi tuwashukuru sana kwa kipindi chote mlichotusikiliza,kuanzia mwezi Septemba mwaka jana hadi mwaka huu mwezi Septemba mwishoni.
Tunashukuru kwa uvumilivu wenu.
Pia tunaomba kumshukuru kaka yetu japo hataki kwa kipindi chote ambacho tumekuwa naye kwenye kesi hii, kwa niaba ya Jamhuri hatukua na nia tofauti zaidi ya kuthibisha shtaka kwa kifungu hiki ambacho ni kwa mara ya kwanza kinakuwa tested.
Jaji: Shtaka limekuwa refu na haya yote lazima tuyasome na tutafakari tunawashukuru pia na wanachi walikuwa wanakuja wakati wote.
Kwa leo tunaishia hapa ushahidi ni mrefu tutahitaji muda wa kutosha ili tuweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake, tutatoa hukumu tarehe sita mwezi wa kumi na moja saa tatu asubuhi.
Katuga: Hati ya mashtaka inasema mshtakiwa aliuchochea umma
Waheshimiwa majaji mtaona kwa mujibu wa kifungu kidogo cha tisa ili mtu ashtakiwe kwa kosa la uhaini ni lazima awe na utii kwa jamuhuri ya muungano na awe ndani au nje ya nchi ya Tanzania.
Na kuwe na nia ya aina yoyote na hati ya mashtaka imechukua false intention to instigate.
Hati ya mashtaka inasema mshtakiwa aliuchochea umma wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Ukiachana na neno did ikachukua neno for the purpose of intimidating the executive na kuacha bunge na mahakama.
Ukiangalia kwenye hati yetu utaona kwamba ile njia aliyoitumia mshtakiwa kudhihirisha njia yake imeachana na maneno kadhaa na hati yetu mashtaka imechukua manifestation by his deed alidhihirisha nia kwa kitendo chake.
Waheshimiwa majaji sehemu zote ambazo nimewaambia tumechukua hili na kuacha hili neno lilotumika maana yake they are not similar, Ili maneno haya yawe sawa lazima kuwe na maneno yanayofanya hivyo mfano neno similar lenyewe au maneno mengine yanayoonesha similarities.
Kwahiyo haya maneno yanayotenganishwa na or hatuwezi kuyatumia yote kwa pamoja kwenye hati ya mashtaka na haya sio maneno yetu na tumetumia neno public ili kufanya hati ya mashtaka iweze kueleweka kulingana na ushahidi ambao upande wa jamuhuri ilitegemea kuutoa.
Maneno haya any person yametoka kwenye kifungu cha tano cha kanuni ya Adhabu, Jamuhuri inamtuhumu mshtakiwa kuchochea Umma kulingana na aina ya maneno yalivyokuwa na hakulenga kikundi fulani au kumlenga mtu fulani.
Ili Jamuhuri ikutaje kwa jina kwa hiyo inatafutwa tafsiri ambayo ita tupa tafsiri ya group of people na hakuna namba kamili ya group of people
kwa hiyo watu watakuwa ni group of people.
Hii sasa tunaipata kwenye tafsiri ya neno public na tafsiri yake tunaipata kwenye kifungu hiki manifestation inaweza kusababishwa kwa kusambaza maandishi au michoro lakini pili kuna ku manifest by overt act
Lakini tatu kuna ku manifest y deer ambapo hati ya mashitaka iliyoko mbele yetu ilionesha kwamba alitamka maneno na kuyasambaza.
Tunasema kwamba kutamka maneno ni kitendo katika tafsiri ya kisheria waheshimiwa majaji na tunalichukua hili kwa kuzingatia kwamba elements za makosa kifungu cha 89 kifungu kidogo cha kwanza.
Mahakama ione kutoa maneno ni kitendo maneno ya kichochezi au lugha chafu na publishing ni kufanya taarifa fulani ijulikane kwa umma
Na tunamtuhumu mtuhumiwa kwa kusema haya maneno akayasambaza na kuyaweka known to the public na mahakama yenu itajiuliza haya maneno ni sentensi iliyokamilika kuleta maana au zisizo na maana.
Waheshimiwa hayo maneno shall be liable sio ya kwangu yamezungumzwa na kesi nyingi.
Preliminary Hearing haitumiki tena na tunaichia sasa jamuhuri jukumu la kuthibisha mashtaka kwa mujibu wa hoja zilizokataliwa.
Na baada ya kuwa tumemaliza hoja kwanza mahakama yenu tukufu tunabaki na hoja mbili tu kama mshtakiwa aliform intention kwa nia ya kuitishia serikali waheshimiwa majaji neno serikali kwenye hati ya mashtaka imetumiwa kuonesha excecutive judiciary na legislature.
Waheshimiwa majaji kwenye kanuni ya adhabu hakuna tafsiri mahususi ya neno executive wala judiciary
Kifungu hiki hakijstoa tafsiri ya hayo maneno kwa kifungu cha 39 kilivyo executive ni executive na neno judiciary and legislature havija define kumaanisha neno tofauti.
Maneno kukinukisha kwa mujibu wa ushahidi wao zililenga kuzuia kupiga kura katika ukurasa wa 619 mshtakiwa akidodosea maswali anasema the executive is responsible kutunza amani na jukumu la kulinda amani ni la polisi chini ya serikali.
Waheshimiwa majaji ushahidi huu unajionesha kilichotishwa ni serikali katika ku maintain peace and order point muhimu ya kuizingatia kwa mujibu wa hati ya mashtaka.
Neno lilitumika aliposema kitanuka kama pilau lengo ni kuitisha serikali wala jamuhuri haipaswi kuthibitisha kama serikali ilitishika au haikutikisika
Katuga: Kauli ya Mshtakiwa ndiyo Iliyotumika kama msingi wa mashtaka ya uhaini
Wakili wa serikali Peter Katuga ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa anakabiliwa na shtaka la uhaini kinyume cha kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya mwaka 2022.
Akiwasilisha hoja zake mbele ya majaji, Katuga amesema kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025 katika eneo la Kinondoni, Dar es Salaam, akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikusudia kuchochea umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katuga amesema upande wa Jamhuri unadai kuwa mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kupitia maneno aliyoyatoa na kuyasambaza, akisema: "Wanasema kitu kimoja sahihi hapa..."
"Maneno hayo ndiyo yaliyochukuliwa na Jamhuri kama kiini cha mashtaka yao," amesema Katuga.
Amefafanua kuwa kifungu cha 39(2)(d) kinaeleza masharti ya kosa la uhaini kwa mtu yeyote aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iwe ndani au nje ya nchi, pale anapotengeneza au kuendeleza nia ya kutenda vitendo vinavyotafsiriwa kuwa vya uhaini.
Katuga pia amenukuu kifungu cha 135 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20, Marejeo ya mwaka 2025, akisema sheria hiyo inaitaka hati ya mashtaka kueleza wazi kosa analoshtakiwa nalo mshtakiwa pamoja na namna kosa hilo linavyodaiwa kutendeka.
"Sheria inataka maelezo ya shtaka yaonyeshe wazi jinsi kosa lilivyofanyika ili mshtakiwa afahamu tuhuma zinazomkabili," amesema.
Aidha, amesema kifungu cha 138(3)(a) cha sheria hiyo kinaelekeza kuwa lugha inayotumika katika hati ya mashtaka inapaswa kuwa ya kawaida, iliyo wazi na isiyoleta mkanganyiko.
Katuga amesisitiza kuwa moja ya masharti muhimu ya kifungu cha 39(2)(d) ni kwamba mtuhumiwa lazima awe mtu aliye chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awe ndani au nje ya mipaka ya nchi.
"Walifungua shtaka la uhaini kwa sababu muhusika alikuwa mtii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kifungu hicho kinavyotaka," amesema Katuga.
Lissu: Kama kuna kosa hukumuni sawasawa na ilivyo kwa mujibu wa sheria
Ushahdi wa kesi hii unasemaje?
Mara tu Chadema na mwenyekiti mshtakiwa na makamu wake walipoanza mkutano ya kuhamasisha no reforms no election msajili aliingilia kati ni ushahdi wa DW2 ni ushahidi wa John Mnyika
na alisema kauli ya no reforms no election ilikuwa kauli ya kisiasa na akatoa taarifa kwa Umma na hiyo kabla ya tarehe tatu April na hiyo inaonesha msajili alikuwa tayari kuingilia na baadaye pia aliandika barua kwangu nikiwa tayari niko nguvuni na kesi ya uhaini.
Nimefunguliwa na hilo suala la msajili kuingilia halimo kabisa na jeshi la mawakili wa serikali na kwa mujibu wa sheria maana huwezi kufungua shauri la jinai kwenye jambo linaloweza kutatuliwa kimadai.
Kesi imefunguliwa bila kufuata sheria sababu walikuwa na haraka ya kuniua na kwa muktadha huo ni rai yangu kwamba mahakama hii itupilie mbali.
Hii kesi imefinguliwa kinyume cha sheria.
Hoja nyingine inayoonesha mashaka makubwa kuhusiana na kesi hii inahusu matumizi ya taratibu za kijanai kuendesha vita ya kisiasa kwa upande wa serikali.
Freeman Haikaeli Mbowe na viongozi wenzake saba wamelipishwa faini ya milioni 350 na mheshimiwa, mashahidi wote wa utetezi walikuja hapa walieleza miaka nenda rudi tunavyotengenezewa kesi wote walieleza walivyowekwa mahabusu wakashtakiwa.
Kesi yangu ya kwanza Christmas’s eve 22 wanangu ilikuwa krisimasi yao ya kwanza na wananiambia baba krisimasi yetu ya kwanza ulikuwa gerezani nimepewa kesi na Kikwete, Magufuli sasa nimepewa kubwa yenyewe na Samia.
Tumeteswa na makesi haya ya kisiasa tunagombania kuhusu mfumo wa uchaguzi sasa matumizi ya mifumo hii ya mashtaka na sheria inaturuhu kuikosoa na kupinga na hatulzimishwi na sheria kuwapenda.
Sheria inaturuhusu kuwa wapinzani na ninaposema sheria namaanisha katiba yetu na penal code inaturuhusu kuipinga kwa kila hali kupinga sera zake mifumo yake bila shida yoyote.
Hata kwenye mambo ya idara ya usalama wa taifa ambayo sheria imesema ni matishio kwa jamuhuri ya muungano, sheria hiyo imeweka wazi tukifanya harakati za kuiondoa serikali kwa kufuata taratibu hilo sio tishio la usalama wa taifa.
Sasa hii mchezo ya kutumia njia za kijinai dhidi ya washindani wa CCM huko sio kutenda haki hiyo ni political percecution.
Sasa waheshimiwa hizi kesi zinatakiwa zipigwe vita na mahakama inasemaje nianze na Freeman Haikael Mbowe mahakama hii ilikabiliwa na shtaka ambalo sio lake alikuwa amesema maneno ya yafuatayo ……Kesho patachimbika akakamatwa akashindwa kesi na mimi nilishtakiwa mara kibao maneno kama serikali imeiba hizo ni tuhuma sasa haziwezi tatuliwa kukamata watu na kuwafunga
serikali ya kidemokrasia lazima ikubali na ivumilie ukosoaji wa kisiasa mimi nimepewa kesi ya uhaini kwa kusema maneno ambayo ni malalamiko ya kiuchaguzi wanataka hawa waendesha mashtaka na mapolisi wao wanataka iwe a police state
kwa msimamo huohuo
Mahakama hii isikubali kuingilia mgogoro wa kisiasa uliogeuzwa kuwa jambo la kijinai.
Hoja yangu ya mwisho kwa mujibu shahidi DW2 aliyesema maneno haya amenifahamu kwa miaka 23 na kwamba ni mashtaka ya uongo mwingine ambaye amenifahamu kwa miaka 20 alisema mimi sio mtu ninayeweza kutenda uhaini
na wote wanasema nimekuwa mhanga wa mabavu ya serikali ya Tanzania na sio rahisi kwa mzalendo kama mshtakiwa kuwa msaliti kwa nchi yake.
Hayo maneno sio ya machawa wangu hao sio machawa hao ni viongozi ambao nimefanya nao kazi nimepambana pamoja nao kupigania nao kupambania nchi yangu na kuthibitisha ushahidi ulioko mahakamani kwa rekodi yangu mbunge kwa kuchaguliwa rais wa TLS mshindi wa tuzo za kimataifa juu ya demokrasia na haki za binadamu.
Umoja wa Mataifa unasema niachiliwe na nilipwe fidia huyu ni mhaini wa aina gani anayepiganiwa na dunia nzima.
Nimepigania haki na demokrasia kwa shemu kubwa ya maisha yangu msimamo huo umenigharimu sana msimamo huo umeniletea madhila mengi sana msimamo huo kwa siku zilizobaki za maisha yangu nitaendelea kuupigania na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao niko tayari kuufia.
Mwisho waheshimiwa majaji namalizia kosa la uhaini halina kosa dogo ambalo ukishindwa kuthibisha uhaini unaadhibu kosa dogo na adhabu yake kufa kunyongwa hadi kufa mzigo ambao uko mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahidi huu mkiona kuna uhaini msigope kuadhibu sawa sawa na ilivyo.
Toeni hukumu inayostahili uhaini na kama hamjaona uhaini msiogope kusema hakuna uhaini hapa mshtakiwa hana hatia.
Kama kuna kosa hukumuni sawa sawa na ilivyo kwa mujibu wa sheria na kama ushahdi haufit basi futulieni mbali huo ni mzigo wa kwenu peke yenu. Mimi nimemaliza.
Tulipoanza niliijulisha mahakama kesi ya uhaini sio kesi rahisi na hata nyie mtakubali ukiachia mbali siasa zake na zinafanya uhaini kuwa kesi ngumu.
Pamoja na magumu yote ya kesi hii, mmetusikiliza mmetupa nafasi ya kujieleza mmenipa nafasi ya kujitetea mmetuvumilia mmefanya kazi nzuri na nilitaka niseme haya sababu sijui kama tutakutana tena kwenye mazingira haya na hawa mawakili wangu wa serikali wamepambana vyovyote mtakavyo amua nawapa pongezi nawatakieni kila la kheri kwenye tafakari yenu.
Ahsanteni sana hayo ndio nilitaka yaingie kwenye rekodi waheshimiwa majaji.
Lissu: Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushahidi wa video
Jaji: Tuendelee
Lissu: Once it is understood haya maneno yanayolalamikiwa kuwa ni ya kihaini yanapoteza hiyo maana mbaya yaliyopewa na upande wa mashtaka.
Ukishaeleza tu mazingira maana ya kihaini yaliyopewa inapotea sababu context inakuwa imeelezea.
Hiyo kwenye context kwa ushahidi wa utetezi ni muhimu kiasi hicho
Na hiyo kinachobaki ni kwenye hayo maneno baada ya kupata ile context kinachobaki ni kile ambacho DW 2 alikisema, alisema hivi ukurasa 679 alisema Maneno …
Waheshimiwa majaji tuhuma inasema mshtakiwa alichapisha hayo maneno kwenye mtandao wa Jambo TV na hayo maneno sio ya kuchapisha ni video mashahidi wote 17 walizungumzia video mashahidi wote watano wa upande wa utetezi vilevile wamezungumzia video.
Waheshimiwa majaji upande wa mashtaka kwenye preliminary hearing waliahidi wataleta video kuja kuthibitisha shtaka lao kwenye list of documentary evidence ukurasa wa 135 kwenye orodha ya vielelezo vinane na tisa walisema wataleta video lakini hawajaleta wameshindwa kutimiza walichoahidi.
Watasema hivi lakini hawa watu wamekubali kuwa hayo maneno yalisemwa na mshtakiwa alikubali na mashahdi wake wakasema hivyo hakuna ubishi kuwa maneno yalisemwa.
Waheshimiwa majaji hiyo hoja wakija nayo sio hoja yoyote yenye maana sababu ya kwanza hakukua na makubaliano kuwa ushahdi uliopo kwenye video umekubalika na pande zote mbili hivyo hauhitaji kuthibitisha hivyo walipaswa walete hiyo video.
Wakati upande wa waleta mashtaka wanasema hayo maneno ni kisa upande wa utetezi umesema throughout hayo maneno sio kosa kwa mujibu wa sheria na msikubali kabisa ushahidi usiokuwa na video, ushahidi mkubwa zaidi ni kwamba mashahidi walijikanganya juu ya urefu wa hiyo video anasema ina saatatu na Dakika 38 na baadaye saa tatu na dakika 45 na huu ni ushahidi wa mtu mmoja.
PW16 anasema hiyo video ilikuwa ndefu na waliangalia kwa takribani kwa saa mbili na dakika kadhaa.
PW17 aliyerekodi na kuirusha anasema video yake ina karibu saa tatu sasa hapa ni ipi ya kwenda nayo hizi ni za upande wa mashtaka kuna version sita na hamjaona hata moja mtaenda na version ipi na kama hiyo haitoshi tuangalie za upande wa defence.
DW, mimi mwenyewe nilisema nilizungumza kwa kati ya saa tatu na tano na kama mazungumzo yangu yalirekodiwa then video yangu ina urefu huo na wengine pia kila mmoja amekuja na muda wake kuna wasaa moja na wengine saa mbili sasa ipi ni sahihi.
DW 5 aliongeza mkorogo zaidi aliona video hiyohiyo jambo tv yenye saa mbili akaona video hiyo chanzo tv yenye dakika 60 na akaona video hiyo The chanzo tv yenye dakika 45 waheshimiwa nani alikuwa na wajibu wa kuthibisha juu ya video? ni upande wa mashtaka hawajathibisha video yoyote just to show how hopeless the case is.
Hicho kipande kina urefu kiasi gani waheshimiwa majaji?.
Waheshimiwa majaji na video hii ilikataliwa na mahakama hii mwezi wa kumi mwaka jana na hawakufanya chochote kurekebisha msiikubali ikataeni.
Waheshimiwa majaji sasa jambo jingine hii kesi imefunguliwa kinyume cha sheria. Jambo likiwa na sura ya kimadai au kijinai lazima zile sura za kimadai zimalizwe kwanza ndipo kesi ya jinai ifunguliwe.
Waheshimiwa majaji ushahidi unasemaje kabla ya ushahidi ni kipi ambacho kina sura ya kiutawala au kimadai waheshimiwa majaji mmeambiwa mara kadhaa mshtakiwa ni mwenyekiti wa chadema chama kilichopo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
Masuala ya vyama siasa na viongozi wao na matendo yao na makosa wakikosea yamekabidhiwa kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa hatua ya kwanza inachukuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na yako kwenye kifungu cha saba cha sheria hiyo.
Lissu:Hakuna ushahdi wa kumfunga mshtakiwa
Jaji subiri kidogo
Jaji: uendelee
Lissu: Waheshimiwa majaji ushahdi unapaswa kuchambuliwa vyema kila mmoja kiundani, nimeuzungumzia ushahidi upande wa mashtaka kwa ujumla wake na vipande vipande vyake nimerejea kesi ya Nguza Viking na Oscar Lwela na ndivyo nilivyofanya waheshimiwa majaji.
"Swali muhimu la kujiuliza ni je, huu ushahidi unalinganishwaje?
Viongozi wa juu viongozi wanaojulikana, viongozi wa juu viongozi wenye sifa njema ndio walikuja kutoa ushahidi mbele yenu waheshimiwa majaji.
DW1, mwanaharakati anayejulilana kwa kupigania demokrasia na haki za binadamu.
Ushahdi wa DW1 na wasifu wake uko kurasa 559 hadi 566 hadi 577 hizo zote zinazungumzia wasifu wa shahdi namba moja wa utetezi.
Jaji: Ndio
Waheshimiwa majaji DW2 katibu mkuu wa Chadema mwanasiasa mbobevu na wasifu wake uko katika kurasa 658 hadi 687 hadi 725 za rekodi za mahakama utaona wasifu wake.
DW3, Amani Sama Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Chadema 729 -730 ushahdi wake uko na 754 hadi 759 na 764 wa rekodi ya mahakama.
DW4, Brenda Rupia, Mkurugenzi wa mawasiliano Chadema miaka 13 ndani ya chama na wasifu wake uko 807-810 814/821 na 827 hadi 828.
Waheshimiwa majaji, D5, John Wegesa Heche na wasifu wake uko katika ukurasa wa 839 hadi 848 hadi 856 na 892 hadi 896.
Waheshimiwa majaji hao ndio walikuja kutoa ushahdi mbele yenu watu wa maana katika siasa na uongozi wa nchi hii, sio watu wa mafIchoni, watu wa maana kabisa.
Mashahidi wote wa upande wa utetezi walikuwa ni mashahidi wa kuona walikuwepo walioona na kusikia kila kilichotokea siku hiyo ulikinganisha na upande wa mashtaka isipokuwa shahidi mmoja ambaye ameungana mkono na mashahidi wa utetezi wote.
Mashahdi wote hawa sio tu walizungumza mambo yaliyotokea tarehe 03/04/ 2025 bali uzoefu wao, matatizo ya kimfumo ya demorasia walizungumza kutoka mioyoni mwao na waliwaambia kila mmoja wao ambavyo wamewahi kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za uongo na kufunguliwa mashtaka na jeshi la Polisi Tanzania, na walizungumza kutoka kwenye uzoefu wao binafsi.
Waheshimiwa majaji viongozi wote hawa waliambia mahakama hii kile ambacho hawakuambiwa na mashahidi wa upande wa mashtaka, context hayo maneno yalizungumzwa mazingira gani na kwanini
Jaji: Ndio
"Waheshimiwa majaji mashahdi wote wale walisema wana maslahi na kesi hii na hawakukana.
Mwenyekiti wao yuko ndani anashtakiwa kwa kisa uhaini.
Ni kiongozi gani ataona mwenyekiti wao yuko ndani na hawakuwa na maslahi na walikuja sababu wanataka haki na ukweli kwa hiyo maslahi yao waliyoyakubali ni maslahi ya kutendeka haki.
Mateso dhidi ya Mwenyekiti wao yakome katiba yao na wale wahalifu waliogeuzwa mashadi walikuja na nia njema ya kusema kweli.
Kwenye kesi, Goodluck Kyando, Mahakama ya rufani ilisema kila shahidi anastahili kukubaliwa ushahdi wake isipokuwa pale palipo na sababu za kutosha za kuukataa ushahidi wake.
Swali langu kati ya ushahdi wa viongozi hawa na wahalifu hawa na mapolisi hawa, mahakama inatakiwa iamini ushahdi upi? ushahidi wa mashahidi hawa walioletwa na mapolisi haustahili kuaminiwa wapo 17 na nataka kumuondoa PW17 kwa sababu ushahidi wake kwa kiasi kikubwa ni ukweli lakini hawa wengine wote hawastahili kuaminiwa hata kidogo na kwa upande mwingine ushahdi wote wa upande wa utetezi unapaswa kuaminiwa na kukubaliwa kwa sababu ambazo nimezieleza kwa kirefu na kwa kusema hayo naomba nisinukuliwe kwamba ushahidi wote wa utetezi haukuwa na mawaaa
Kwa Mungu huko ndio ushahidi unakuwa spotless lakini duniani hapa ni ushahidi wa binadamu hivyo dosari hazikosekani.
Nitoe mfano waheshimiwa majaji mashahidi wengi wa utetezi pamoja na mimi tuliburuzwa sana kwenye cross examination na waliweza sana kuonesha madhaifu ya utetezi wetu,kuna shahidi aliulizwa una magari mangapi akasema mawili akaoneshwa ana magari matano ninachotaka kusema kwenye ushahdi wa msingi walikuwa thabiti kasoro kwenye masuala ambayo hayahusiani na kesi hii na hayaamui kesi hii.
Kwa hiyo ninaposema ushahidi wao nina maana hiyo. Nguza Viking Babu Seya mahakama ilisema nini juu ya discrepancies
Jaji Natalia Kimaro Mahakama ilisema hivi hukumu haitatolewa kutokana na contradictions na kipimo ni ushahidi usio na udhaifu wa namna yoyote na hayo mengine yanaisaidia mahakama tu kuthibitisha ushahidi wao huo.
Msimamo wa kesi ya Babu Sea pia uko kwenye kesi ya Mohamed Haruna Supra kesi ya Vitalis Joseph Supra
waheshimiwa majaji nimemaliza kuusemea ushahidi na kwa ushahidi huu hakuna ushahdi wa kumfunga mshtakiwa badala yake kuna ushahdi wa kutosheleza kumuachia mshtakiwa.
Pia naomba niongeleee eneo jingine linaloleta mashaka katika kesi hii waheshimiwa.
Mashaka makubwa na ya msingi, mashaka ni jinsi upande wa mashtaka umejaribu kuficha mambo muhimu kwenye hiyo hotuba ya tarehe 3/4/2026 na kesi imetengenezwa kwa kunyofoa maeneo mengi ambayo kama yangekuwepo yangeonesha hakuna kesi wamefanya cherry picking maneno waliyotaka na wasiyotaka yaingine kwenye hati ya mashtaka ionekane kuna mambo makuuuuubwa yalifanyaka hiyo siku ya mkutano.
Sababu ya kuokota okota tu maneno naomba kwa ridhaa yenu ni warudishe katika hati ya mashtaka kwenye hayo maneno wanayolalamikia ukiangalia hayo maneno kwa makini unabaini kwamba kuna mambo wameyaondoa wanasema msimamo huu una ashiria uasi ni kweli sababu ………. sababu tunaenda kukinukisha sana sana.
Hayo ndio maneno mtu asiye makini ataona shida inaanza kabla ya neno la kwanza kuna zile doti tatu zina maana kwamba kulikuwa na maneno kabla wanasema kitu kimoja sahihi hapa hayo maneno ya kabla yameondolewa na uthibitisho ni hizo alama.
Baada ya neno mabadiliko kuna alama hizohizo tena, kuna maneno yameondolewa hayo yaliyokuwepo
kabla ya wanasema ni maneno gani yalikuwa na maaana gani na kwanini yameondolewa.
Hivyohivyo kwenye maneno mengine kuna maneno yalikuwepo pia kati ya kukinukisha na sasa yameondolewa kwani yameondolewa huu uchaguzi tutauvuruga kuna maneno yaliyofuata yameondolewa ni maneno gani na kwanini yaondolewe.
Kwa kuangalia hati ya mashtaka hakuna mtu anaweza kupata majibu yake na waleta mashtaka hawajaleta majibu yoyote juu ya meneno hayo.
Waheshimiwa majaji facts are stubborn ukweli una tabia ya ubishi na huwa unakataa kufichwa.
Ukweli ni mgumu kama jiwe hicho ambacho kimefichwa kimeletwa kwenye ushahidi, kile ambacho hati ya mashtaka haikutaka mjue.. kwanza, hii kesi ni kunusu mgogoro wa kisiasa kwa zaidi ya mika 30, ni mgogoro wa kikatiba kubusu chaguzi za nchi hii, mgogoro kati ya Chadema na CCM na serikali.
Kielelezo D16 kinaonesha ni
mgogoro wa kiuchaguzi. Ushahidi ulitolewa na mashahdi wote mashahdi 17 na mashahdi wa utetezi ni ushahidi unaonesha ni mgogoro wa kisiasa kuhusu uchaguzi huo ni muktadha muhimu katika kuelewa hii kesi
Mgogoro huu umekuwa unapiganiwa kwenye majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari sasa huu mgogoro, serikali na mapolisi wameuvalisha vazi sasa kuwa ni mgogoro wa kijinai.
Katika ushahdi wa pande zote mbili ushahidi wa upande wa utetezi ndio umetoa muktadha sahihi wa kesi hii.
DW4 alituambia wanasema hai hii inashiria uasi, je ni akina nani?
Ni shahidi huyu ndio alitupa lawama wanaosema ni G55 hawakutuoa maana ya kukinukisha bali tumeipata kwenye ushahidi wa utetezi kwa jinsi walivyoandaa hati ya mashtaka na kunyofoa.
Wanajaribu kuonesha kuna kosa kubwa sana limefanyika hapa na context yote tumeipata kwenye ushahidi wa utetezi.
Ushahidi wa utetezi umetupatia missing context hicho ambacho upande wa mashtaka haukutaka kijulikane kwa kunyofoa nyofoa maneno na kimejulikana kwasababu ya ushahidi wa utetezi
Waheshimiwa majaji.
Tutafakari yaliyo katika ushahidi wa PW1
Jaji kwani tusiende break afu ndio unamalizia
Lissu.
Lissu: Majaji wafuate kauli ipi, kupindua au kuitishia serikali?
Tundu Lissu, anaendelea kuhoji uaminifu wa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, akidai kuwa mashahidi wa siri waliotumika katika kesi hiyo walikuwa na maslahi binafsi na hivyo ushahidi wao haupaswi kupewa uzito bila kuungwa mkono na ushahidi mwingine huru.
Akiwasilisha hoja zake kwa majaji, Lissu amesema ushahidi uliotolewa na maofisa wa polisi walioongoza uchunguzi wa kesi hiyo una mkanganyiko mkubwa kiasi cha kuzua shaka iwapo walikuwa wakizungumzia kesi moja.
“Kwa kulinganisha ushahidi wao, mtu hawezi kukubali kwamba maofisa hawa wawili wa polisi wanazungumzia kesi moja. Kwa kutumia akili ya kawaida tu, mtu hawezi kusema ni kesi moja,” amesema Lissu.
Amedai kuwa shahidi wa 16 (PW16) alitoa maelezo yanayokinzana na hoja za upande wa mashtaka kwa kudai kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuipindua Serikali, wakati hati ya mashtaka inadai lengo lilikuwa kuitishia Serikali.
“PW16 anasema mshtakiwa alikuwa na lengo la kuipindua Serikali, huku mashitaka yakisema ilikuwa ni lengo la kuitishia Serikali. Kupindua Serikali ni kesi tofauti kabisa na kuitishia Serikali. Sasa mtaenda na kauli ipi waheshimiwa majaji?” amehoji.
Lissu pia amepinga madai ya kuwapo kwa mwanasheria aliyeshirikishwa katika uchunguzi huo, akisema hakuna ushahidi unaothibitisha ushiriki wake.
“PW16 alisema kulikuwa na mwanasheria, lakini hakutaja jina lake. Kwenye vielelezo hakuna maelezo yoyote ya mwanasheria huyo, na hakuna mwanasheria aliyekuja hapa kutoa ushahidi. Hayo ni maelezo ya polisi ambayo hayajathibitishwa,” amesema.
Aidha, amedai kuwa PW16 alitoa maelezo yanayokinzana kuhusu ushirikishwaji wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akiwataja baadhi ya watu waliodaiwa kuhusika katika uchunguzi bila kuitwa mahakamani kuthibitisha madai hayo.
“Akasema aliwasiliana na Ofisi ya DPP kupitia mtu anayeitwa Mayenda, lakini huyo Mayenda hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi. Hayo yanabaki kuwa maneno ya shahidi pekee,” amesema.
Akizungumzia mashahidi wa siri, Lissu amesema wengi wao walikamatwa kwa tuhuma za kupanga vitendo vya uhalifu kabla ya baadaye kugeuzwa mashahidi wa upande wa mashtaka.
“Walikamatwa, wakaandikishwa maelezo kama mashahidi na baadaye wakaletwa mahakamani kwa kificho. Hawa si mashahidi huru, ni watu waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma na baadaye wakawa mashahidi wa upande wa mashtaka,” amesema.
Kwa mujibu wa Lissu, mashahidi hao walikuwa na maslahi binafsi katika kesi hiyo na hivyo ushahidi wao ulipaswa kuungwa mkono na ushahidi mwingine wa kujitegemea.
“Ushahidi wa mtu mwenye maslahi binafsi unapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa na hautakiwi kutumiwa isipokuwa kama umeungwa mkono na ushahidi mwingine huru,” amesema, akirejea maamuzi mbalimbali ya Mahakama ya Rufani.
Amedai pia kuwa hakuna hata mmoja wa mashahidi hao aliyedai kutishiwa maisha yake au ya familia yake, jambo ambalo kwa maoni yake linaibua maswali kuhusu matumizi ya utaratibu wa ushahidi wa siri.
“Niliwauliza kama walitishiwa maisha yao au ndugu zao wakatishiwa, wote wakasema hapana. Sasa msingi wa kuwaficha ulikuwa upi?” amehoji.
Lissu ameendelea kuhoji uaminifu wa baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka, akidai walitoa maelezo yanayokinzana kuhusu taarifa zao binafsi, ikiwemo dini, kazi na uanachama wao wa kisiasa.
“PW5 alitoa maelezo yanayokinzana hata kuhusu dini yake. Mtu anayetoa maelezo tofauti kuhusu jambo la msingi namna hiyo, mahakama inapaswa kuupima ushahidi wake kwa umakini mkubwa,” amesema.
Kwa mujibu wa Lissu, kati ya mashahidi wa siri walioitwa na upande wa mashtaka, wengi wao walikuwa mashahidi wenye maslahi binafsi na hakuna ushahidi huru uliowasilishwa kuthibitisha madai yao.
“Katika mashahidi wa siri walioitwa, wengi wao ni mashahidi wenye maslahi. Ushahidi wao haujathibitishwa na ushahidi mwingine huru. Huo ndio ushahidi ambao upande wa mashtaka unatarajia mahakama iutegemee,” amesema.
Lissu amehitimisha kwa kueleza kuwa ushahidi wa shahidi wa 17 (PW17), kwa mtazamo wake, uliunga mkono hoja za utetezi badala ya kuimarisha kesi ya upande wa mashtaka.