Je, hatima ya Netanyahu ni ipi Eisenkot akiunda serikali?

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Rais wa Israel, Isaac Herzog, amempa kiongozi wa upinzani, Gadi Eisenkot, nafasi ya kwanza ya kujaribu kuunda serikali mpya ya mseto, baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita kushindwa kumpa upande wowote wingi wa viti bungeni.

Eisenkot sasa ana siku 28 za kujaribu kupata uungwaji mkono wa kutosha kuunda serikali, huku akiwa na uwezekano wa kuongezewa siku nyingine 14.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, mkuu huyo wa zamani wa jeshi alisema: "Sasa ni wakati wa kuunda serikali ya dharura ya kitaifa. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha tunakabiliana na hali hii ipasavyo."

Uamuzi wa Herzog umefuatia mashauriano yake na wawakilishi wa vyama vya siasa. Kulingana na taarifa kutoka Ofisi ya Rais, Eisenkot alipata uungwaji mkono wa wabunge 67, dhidi ya 46 waliomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu.

Rais ana mamlaka ya kumteua mtu anayemwona kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuunda serikali. Haimlazimu kumchagua kiongozi wa chama kilichopata viti vingi zaidi bungeni.

Hesabu ya viti bungeni

Chama cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu pamoja na washirika wake wenye misimamo mikali kina viti 53 kati ya 120 katika bunge la Israel, Knesset.

Kwa upande mwingine, chama cha Eisenkot pamoja na vyama vingine vitatu vya upinzani vya Kiyahudi vina viti 48.

Miungano miwili inayowakilisha Waarabu wa Israel ina jumla ya viti 19. Matokeo hayo yanaviweka vyama hivyo katika nafasi muhimu ya kuamua ni nani atakayeunda serikali ijayo.

Kufuatia mashauriano na wawakilishi wa wabunge waliochaguliwa hivi karibuni, Eisenkot alipata uungwaji mkono wa wabunge 67, huku Netanyahu akipata 46.

Rais ana mamlaka ya kumchagua mtu anayemwona kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuunda serikali; hana wajibu wa lazima wa kumchagua kiongozi wa chama chenye idadi kubwa zaidi ya viti bungeni.

Matokeo ya uchaguzi yanatoa chaguzi tatu zinazowezekana kwa ajili ya kuunda serikali: serikali ya umoja wa kitaifa inayowajumuisha wote wawili, Netanyahu na Eisenkot; muungano wa vyama vyenye misimamo mikali, Netanyahu, na watu waliohama kutoka chama cha Eisenkot; au serikali inayoongozwa na Eisenkot kwa kuungwa mkono na vyama vya Waarabu.

Hata hivyo, vyama vingi vya Kiyahudi vilikuwa vimeahidi kabla ya uchaguzi kutounda serikali pamoja na vyama vya Waarabu.

Ingawa Eisenkot na wanachama wote wa chama chake wamekataa wazo la kushirikiana na vyama vya Waarabu, inaaminika kuwa kuna uwezekano wa kufikia makubaliano.

Vinginevyo, anaweza kujaribu kufikia makubaliano na vyama vyenye misimamo mikali, ingawa huenda akakabiliwa na changamoto kubwa katika kufanya hivyo.

Ni upi mustakabali wa Netanyahu?

Profesa Tukur Abdulkadir, mtaalamu wa siasa za kimataifa na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Kaduna, amesema hali hiyo haikuwa ya kushangaza kabisa, lakini bado ni vigumu kutabiri nani atafanikiwa kuunda serikali.

"Hali hii ilitarajiwa kwa kiasi fulani; hata hivyo, ni vigumu kutabiri kama atakuwa Netanyahu, Eisenkot, au mtu mwingine yeyote atakayeibuka ingawa hakuna kati ya hayo litakaloshangaza.", alieleza Profesa Takur.

Amesema mgawanyiko kati ya Eisenkot na Netanyahu umeongeza utata katika mchakato huo, licha ya wawili hao kuwahi kufanya kazi pamoja.

Kwa mujibu wa Profesa Abdulkadir, tofauti hizo zinahusu zaidi masuala ya itikadi za Kiyahudi kuliko haki na uhuru wa Wapalestina.

Profesa huyo aliongeza, "Mwishowe, inawezekana kuundwa kwa serikali ya mseto, ambayo inaweza hata kujumuisha vyama vya siasa vya Waarabu."

"Ikiwa upinzani utaunda serikali nchini Israel na kwa kuzingatia hali ya sasa ya kisiasa nchini Marekani, ambapo wanachama wengi wa Chama cha Democratic hawungi mkono vita kuna uwezekano kuwa msimamo wa Israel unaweza kubadilika. Hii inaweza kuathiri hasa migogoro yake inayohusisha Wapalestina, Iran, na Lebanon, ikizingatiwa kuwa Marekani ndiyo mshirika mkuu wa Israel," alibainisha Profesa Abdulkadir.

Je, kumewahi kuwa na serikali ya mseto?

Kuna mfano wa awali wa kuundwa kwa serikali ya mseto. Mnamo mwaka 2020, kufuatia chaguzi tatu zilizotoa matokeo yaleyale, Netanyahu na mpinzani wake wa mrengo wa kati, Benny Gantz, walikubaliana kugawana madaraka.

Wakati akifanya mashauriano na vyama vya siasa, Herzog alisema kuwa ili kuepuka duru nyingine ya uchaguzi na kufanikiwa kuunda serikali imara, "vyama na wawakilishi wao lazima waelewe kuwa si kila ahadi inaweza kutimizwa."

Kati ya mwaka 2019 na 2022, siasa za Israel zilikumbwa na mgawanyiko mkubwa, huku chaguzi tano zikifanyika wakati Netanyahu na wapinzani wake wakijaribu kuunda serikali ya mseto.

Je, Eisenkot anaweza kuunda serikali ya mseto?

Eisenkot sasa ana siku 28 za kujaribu kuunda serikali mpya, huku akiwa na uwezekano wa kuongezewa siku nyingine 14 iwapo ataomba muda zaidi.

Akizungumza kupitia mtandao wa X, mkuu huyo wa zamani wa jeshi alisema: "Sasa ni wakati wa kuunda serikali ya dharura ya kitaifa. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha tunastahili kupewa jukumu hili."

Israel haijawahi kuwa na chama kimoja cha kisiasa kinachomiliki wingi wa viti bungeni. Hivyo, serikali zake zimekuwa zikitegemea miungano ya vyama mbalimbali.

Chama cha Likud kinachoongozwa na Benjamin Netanyahu, pamoja na washirika wake wenye misimamo mikali na vyama vya Kiyahudi vya Kiorthodoksi kali, kina viti 53 kati ya 120 katika bunge la Knesset.

Kwa upande mwingine, chama cha mrengo wa kati cha Eisenkot, pamoja na vyama vingine vitatu vya upinzani vya Kiyahudi, vina viti 48.

Miungano miwili ya kisiasa inayowakilisha Waarabu wa Israel, United Arab List na Joint List, ilipata jumla ya viti 19. Haya ni matokeo yanayovipa vyama hivyo nafasi muhimu katika mazungumzo ya kuunda serikali.

Hata hivyo, karibu vyama vyote vya Kiyahudi, isipokuwa kimoja, vilikuwa vimeahidi kabla ya uchaguzi kutounda serikali ya mseto na vyama vya Waarabu.

Rais Isaac Herzog alisema kuwa baada ya kufanya mashauriano na vyama vyote vya kisiasa kwa wiki moja, aliamua kumpa Eisenkot fursa ya kwanza ya kujaribu kuunda serikali.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais ilithibitisha kuwa Eisenkot na Netanyahu wote wamejulishwa kuhusu uamuzi huo.